Viwanda vya kutengeneza silaha vya Korea Kaskazini vinafanya kazi kamili ya kutengeneza silaha na makombora kwa ajili ya Urusi, huku vita vikali vya Moscow nchini Ukraine vikiendelea hadi sasa kuwa mwaka wa tatu kulingana na waziri wa ulinzi wa Korea Kusini,.
Makadirio ya hivi punde kutoka Korea Kusini yanatoa dalili mpya juu ya jukumu muhimu lakini la usiri sana ambalo Korea Kaskazini inacheza kusaidia kuzuwia tena vita vya Moscow wakati ambapo hitaji la Ukraine la ugavi muhimu wa kijeshi linashikiliwa na wabunge wengi wa Republican mjini Washington.
Silaha na zana za kijeshi, ambazo ni pamoja na mamilioni ya mizinga , zinawasilishwa Urusi kwa kubadilishana na usafirishaji wa chakula na mahitaji mengine, Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini Shin Won-sik alisema Jumatatu.
Kulingana na CNN tangu Agosti, Pyongyang imesafirisha takriban kontena 6,700 hadi Urusi, ambazo zinaweza kuchukua zaidi ya raundi milioni 3 za makombora ya milimita 152 au zaidi ya raundi 500,000 za kurusha roketi nyingi za mm 122, kulingana na wizara ya Shin.
Kwa kubadilishana, chakula kinachangia sehemu kubwa zaidi ya kontena kutoka Urusi hadi Korea Kaskazini, na hali ya usambazaji wa chakula katika taifa hilo lililojitenga la Asia inaonekana kuwa “imara,” kulingana na wizara ya ulinzi.