Korea Kaskazini imeidhinisha mkataba wa kihistoria wa ulinzi wa pande zote na Urusi, vyombo vya habari vya serikali vimetangaza, huku wasiwasi wa kimataifa ukizidi kuongezeka kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Moscow na Pyongyang.
Kim Jong Un, kiongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea – jina rasmi la Korea Kaskazini – alitia saini amri ya kuidhinisha Mkataba wa Ushirikiano wa Kikakati Kamili na Urusi siku ya Jumatatu.
Makubaliano hayo yataanza kutekelezwa wakati pande zote mbili zitakapobadilishana hati za uidhinishaji, kulingana na shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini, KCNA.
Mkataba huo, uliotiwa saini kwa mara ya kwanza mjini Pyongyang mnamo Juni 19 wakati wa ziara ya kifahari ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, unazilazimisha nchi zote mbili kutoa usaidizi wa kijeshi wa haraka kwa kila mmoja kwa kutumia “njia zote” muhimu ikiwa moja inakabiliwa na “uchokozi”.
Alipoafiki makubaliano hayo na Putin mwezi Juni, Kim alipendekeza makubaliano hayo kama hatua ya kuinua uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kuelezea mapatano hayo ya kijeshi kama kitu sawa na “muungano” kati ya Urusi na Korea Kaskazini.
Bunge la Urusi liliidhinisha mkataba huo tarehe 6 Novemba kuongezeka kwa ushirikiano wa usalama na Korea Kaskazini ikiwa ni pamoja na kuripotiwa kwa uhamisho wa silaha kwa Urusi na kutumwa kwa maelfu ya wanajeshi wa Korea Kaskazini kusaidia vita vya Urusi nchini Ukraine.