Shule mbalimbali zimefunguliwa kwenye bara la Asia huku Korea Kusini ikiwa miongoni mwa Nchi zilizofanya maamuzi hayo baada ya kuzifunga Shule hizo kwa muda wa miezi mitatu.
Mpaka sasa Nchi hiyo ina Wagonjwa zaidi ya elfu kumi na moja na vifo zaidi ya 250 vilivyotokana na virusi vya corona ambapo hata hivyo saa kadhaa baada ya kufungua Shule Nchi nzima, kuna baadhi ya Shule zilifungwa huko Incheon jiji lilolo karibu na Mji mkuu wa Seoul baada ya Wanafunzi wawili kukutwa na corona.
Shule mbalimbali zimechukua tahadhari baada ya kufunguliwa ambapo kabla Wanafunzi hawajaingia darasani wanapimwa kwanza joto la mwili na wanahimizwa kukaa umbali wa mita moja hadi mbili kati ya Mtu na Mtu na kutofanya mikusanyiko, kwenye hii picha hapo juu ni Wanafunzi wakiwa wanakula chakula cha mchana Shuleni.
Jeonmin high School iliyopo Daejeon imeamua kuweka uzio wa plastiki kati ya Mwanafunzi na Mwanafunzi wakati wa kula ikiamini ni njia sahihi za kuwakinga na kirusi corona kama inavyookana kwenye picha hapo juu.
Korea Kusini imewaruhusu Wanafunzi wa Sekondari pekee kurudi shule kwa sasa ambapo wa primary na madaraja ya chini wameambiwa waendelee kubaki nyumbani hadi June 8 2020.