Korea Kusini imepiga kura ya kumuondoa madarakani kaimu rais wake wiki mbili baada ya bunge kupiga kura ya kumshtaki rais wake Yoon Suk Yeol.
Jumla ya wabunge 192 walipiga kura ya kung’atuliwa kwake, zaidi ya kura 151 zinazohitajika ili kufanikiwa.
Waziri Mkuu Han alichukua wadhifa huo baada ya Rais Yoon kuondolewa madarakani na bunge kufuatia jaribio lake lisilofanikiwa la kuweka sheria ya kijeshi tarehe 3 Disemba.
Han alitakiwa kuiongoza nchi hiyo kutoka katika msukosuko wake wa kisiasa, lakini wabunge wa upinzani walidai kuwa alikuwa akikataa matakwa ya kukamilisha mchakato wa kumuondoa Yoon.
Ilikuwa ni eneo la machafuko bungeni huku kura ikipigwa siku ya Ijumaa.
Wabunge kutoka chama tawala cha Yoon na Han cha People Power Party (PPP) waliandamana baada ya spika wa Bunge la Kitaifa Woo Won-shik kutangaza kuwa ni kura 151 pekee ndizo zitahitajika ili kupitisha mswada wa kuondolewa madarakani.
Hii ilimaanisha kuwa, tofauti na kura 200 zinazohitajika kwa kuondolewa kwa Yoon, hakuna kura kutoka kwa wabunge tawala ambazo zingehitajika wakati huu kwa Han kushtakiwa bungeni.
Wabunge wa chama tawala walikusanyika katikati ya ukumbi wa kupigia kura wakiimba, “batili!” na “matumizi mabaya ya madaraka!” akijibu, na kumtaka Spika aondoke madarakani. Wengi wao walisusia kura.
Han atasimamishwa kazi mara tu atakapoarifiwa rasmi na bunge.
Kama Yoon, kuondolewa mashtaka kwa Han kutahitaji kuthibitishwa na mahakama ya kikatiba, ambayo ina siku 180 kutoa uamuzi kuhusu iwapo mashtaka hayo yanapaswa kuzingatiwa.
“Ninaheshimu uamuzi wa Bunge la Kitaifa,” Han alisema Ijumaa, akiongeza kwamba “atasubiri uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba