Ikulu ya Kremlin imekataa kuzungumzia madai ya serikali ya Marekani kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un anatarajiwa kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin nchini Urusi ili kuendeleza mazungumzo ya silaha kati ya nchi hizo mbili.
“Hatuna la kusema juu ya mada,” msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema Jumanne.
Baraza la Usalama la Kitaifa la Washington lilionya Jumatatu kwamba majadiliano ya silaha kati ya Moscow na Pyongyang “yanaendelea kikamilifu.”
“Tuna habari kwamba Kim Jong Un anatarajia majadiliano haya kuendelea, kujumuisha ushiriki wa kidiplomasia wa ngazi ya kiongozi nchini Urusi,” msemaji wa baraza hilo Adrienne Watson alisema katika taarifa.
Gazeti la New York Times liliripoti kwa mara ya kwanza mkutano unaowezekana kati ya Kim na Putin nchini Urusi, likisema unatarajiwa kufanyika mwezi huu.