Baada ya Kampuni ya UDA-RT kuwasilisha maombi ya nauli zitakazotumika kwa mabasi yaendayo haraka kwa Mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) May 09 206 SUMATRA imetangaza nauli hizo.
SUMATRA imesema kuwa njia ya pembezoni (Freeder Route) nauli ya mtu mzima ni 400 na mwanafunzi 200 na njia kuu (Trunk Route) ni tsh 650 na mwanafunzi 200.
Njia kuu+pembezoni nauli ni 800 na mwanafunzi 200 mfano njia kuu yaani kutoka Kimara mpaka kivukoni nauli itakuwa 650 na ukitoka mbezi mwisho mpaka kivukoni (hapo umechukua njia ya pembeni ukaunganisha na njia kuu) nauli itakua 800, ukitoka Morroco mpaka kariakoo au kivukoni nauli itakuwa 650 mwanafunzi 200.
Huduma hiyo itatolewa kuanzia kesho bure kwa wananchi kwa siku mbili na May 12 2016 zitaanza kutozwa nauli zilizotajwa.
Msimamizi wa mradi kutoka DART, Eng Ronald Lwakatare amesema……….>>>‘Wakati huo tunafanya majaribio tutakuwa tunaangalia mfumo unavyofanya kazi kwa hiyo tutawabeba abiria kwa siku kadhaa bila kulipa nauli’
ULIKOSA MABASI YAENDAYO HARAKA YALIPOTAMBULISHWA KWA MARA YA KWANZA? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE