Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Ruhinda Mugalulo mkoani Kagera ametiwa mbaroni baada ya kufika katika kijiji cha Rukoma na kuitisha mkutano wa hadhara ikiwa ni sambamba na kuwachangisha wananchi fedha kwa madai ya kuwafanyia tathmini ya kufungiwa umeme wa REA awamu ya tatu akijitambulisha kama Afisa wa mradi wa umeme vijijini {REA}.
Kutoka TANESCO Kagera, Msimamizi wa mradi wa umeme vijijini {REA} wilaya ya Bukoba Thobias John amesema kuwa walifika katika eneo hilo la mkutano baada ya kupewa taarifa mwanakijiji.
Walipofika walimkamata na kumhoji na akakiri kuwa ni kweli yeye hatoki TANESCO ndipo wakabaini moja kwa moja kuwa ni tapeli na alitaka kuwaibia wananchi.
Watu wanne wamekamatwa Arusha kwa kumteka Mwandishi wa habari