Leo December 28 2016 Tume ya kudhibiti UKIMWI TACAIDS kupitia kwa mkurugenzi Mtendaji wake, Dkt Leonard Maboko amezitoa takwimu za hali ya VVU na UKIMWI Tanzania kulingana na hali Duniani na ya ukanda wa mashariki na kusini mwa Afrika, Taarifa aliyoitoa Dkt Maboko imeyaeleza haya……
1.Watu waishio na VVU kwa mwaka 2015 Tanzania walikuwa takribani milioni 1.4.
2.Watu wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU hadi kufikia June 2016 Tanzania walikuwa takribani 800,000.
3.Inakadiriwa mwaka 2015 nchini Tanzania kati ya watu 54,000 waliambukizwa virusi vya UKIMWI.
4.Kiwango cha maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kimeshuka kwa zaidi ya 20% kati ya mwaka 2010- 2015
VIDEO: Madereva walioongoza kwa Ulevi Dsm Christmas hii, Bonyeza play hapa chini