Shirika The Mines Advisory Group linalopinga matumizi ya mabomu yanayotegwa ardhini limesema kuwa limetegua mabomu zaidi ya 9,000 katika miezi sita iliyopita, katika maeneo ambayo yalikuwa yamedhibitiwa na Islamic State nchini Iraq na Syria.
Shirika hilo linasema zinahitajika dola milioni 100 zaidi, kutegua mabomu mengine yaliyotegwa hivi karibuni na mengine yaliyobaki kutokana na vita za zamani.
Shirika limetoa wito huo ikiwa imetimia miaka 20 tangu hayati Princess Diana kuzuru maeneo yaliyozikwa mabomu huko Angola ziara iliyosaidia ulimwengu kujua kuhusu tatizo hilo.
VIDEO: Askari Magereza walivyoonyesha uwezo wao mbele ya Waziri Nchemba, Bonyeza play hapa chini kutazama