Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za Mafuta ya Petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano August 02, 2023 saa 6:01 usiku ambapo kwa mwezi Agosti 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam Petrol ni Tsh. 3199 kwa lita, dizeli Tsh. 2935 na mafuta ya taa 2668.
Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Agosti 2023 yaliyoonesha kupanda kwa bei yanatokana na Changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.