Watanzania wameshauriwa kuandika wosia kabla hawajafariki na wasiwe na dhana kwamba kuandika wosia ni kujichulia kifo badala yake watambue kuwa wosia unasaidia kuondoa migogoro ya Kifamilia pale Mtu anapofariki kwakuwa wosia unaonesha nani atasimamia mali za marehemu na Warithi wake watakuwa ni nani, hivyo inaepusha migogoro ya Watu kugombea mali.
Hayo yamesemwa na Irene Nyantori ambaye ni Wakuli wa Serikali Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa muendelezo wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) kwa Mkoa wa Ruvuma ambapo Wataalamu wanaendelea kutembelea maeneo mbalimbali kutoa elimu na jana walikuwa Mtaa wa Makambi Kata ya Ndirima Litembo.
“Tunawaelimisha Watu zaidi kuhusiana na wosia na kuandika wosia kwasababu unapoandika wosia unaondoa matatizo mengi sana Mtu akifariki kwasababu wosia unaonesha nani atasimamia mali za marehemu, Warithi wake watakuwa ni nani, hivyo inasaidia migogoro ya Watu kugombea mali”
“Watu waandike wosia na wasiwe na dhana kwamba kuandika wosia inaweza kufanya Mtu aone kwamba ndio nakufa hapana, tunawapa wito Watu waandike wosia”
“Tuna banda letu Majimaji Songea Mtu yoyote anayetaka kuandika wosia afike kwenye banda letu tuna Wanasheria pale, pia tunawaelimisha Wananchi wakiandika wosia kwakuwa ni urithi anaweza kwenda kuuhifadho ofisi za RITA, Kanisani, Msikitini au kwa Mawakili”