Licha ya Serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji kwa asilimia mia na kupitia Mpango wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani wa kumtua ndo kichwani mama Changamoto ya uulinzi wa miundombinu ya maji pamoja watu kugoma kuchangia huduma hiyo kumetajwa kuwa ni chanzo ambacho kunadhoofisha ubora wa miundombinu hiyo
Hayo yamesemwa na Afisa tawala ofisi ya mkuu wa wilaya ya kilosa Angela Mono kwaniaba ya mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka katika mkutano wa wadau wa sekta ya maji.
Angela Mono amesema kuwa Serikali imewekeza pesa nyingi kuhakikisha wananchi wanapata maji hivyo ni jukumu la Kila mwananchi kuhakikisha analinda na kutunza vyanzo vya maji sambamba na kuchangia fedha
Kwa Upande wake Meneja wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA)Mkoa Morogoro Mhandisi Sospeter Lutonja amesema kuwa kipimo Cha wadau wanaohusika na maji ni kuangalia miradi iliyowekwa na Serikali yote inafanya kazi kwa uhakika na kuviagiza vyombo vyote vinavyohusika na maji kusimamia miradi hii ili iendelee kutoa huduma