Kuelekea siku ya haki ya mlaji duniani tume ya ushindani nchini FCC,inatarajia kuendesha clinic maalumu ya walaji ama wateja wa huduma mbalimbali katika mikoa ya Dodoma ,Mwanza,Arusha na Mbeya ambapo tume hiyo itawasilikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazo mkabili mlaji sambaba na kuwapa elimu bora ya kutatua changamoto au matatizo.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa FCC Wiliam Erio katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam leo katika kuutaarifu umma kuhusu uzinduzi wa siku ya kumlinda mlaji duniani ambapo,amesema clinic hiyo inatarajiwa kufanyika tarehe 13 mwezi huu,ambapo lengo kuu ni kuhakikisha kumlinda mlaji kupata huduma na kumpatia bidhaa bora.
Pia aliongeza kwa kutoa wito kwa wananchi wanaochukua mikopo ya kausha damu kuwa waachane na mikopo hiyo na wafwate taasisi husika au rasmi zilizoruhusiwa kutoa mikopo ili waweze kupata mikopo isioumiza.