Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Chama cha Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) kimewata wadau wa maendeleo nchini kuendelea kuigusa jamii moja kwa moja hasa kwa wenye uhitaji sambamba na kumuunga mkono Mhe. Rais Samia katika uwekezaji hasa sekta ya Afya.
Ameyasema hayo leo katika hospital ya Mwabepande, Kinondoni Jijini Dar es Salaam wakati TUGHE wakiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kupeleka mahitaji katika hospital ya hiyo, Mwenyekiti Kamati ya Wanawake mkoa Dar es salaam (TUGHE), Bi Jojina Chirwa amesema maadhimisho hayo yanawapa nafasi ya kutafakari kwa ujumla kuhusu changamoto zinazotokana katika jamii na kuwafikia zaidi wenye uhitaji na kuweka mikakati ya namna ya kuzitatua.
Aidha amesema mpaka sasa kumekuwa na mafanikio makubwa katika Taasisi ya Tughe kwa sababu ya kusimamia haki na misingi bora, mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanaoshiriki katika matukio mbalimbali ya TUGHE pamoja na kujua nini tunafanya na malengo yetu ni yapi.