Kuelekea sikukuu ya Eid al Fitr Jeshi la Polisi limewataka madereva Mikoa yote nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali.
“Ni wito wa Jeshi la Polisi kwa madereva wote kuepuka kutumia kilevi na kutaka kuendesha gari, Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha usalama wa raia na mali zao, hivyo likimbaini dereva aliyetumia kilevi, litamkamata, litampima kiwango cha ulevi na kumchukulia hatua za kisheria ikiwemo kumfikisha mahakamani na kumfungia leseni yake”
Taarifa ya Msemaji wa , Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime ameeleza hayo katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habari.