Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), imetahadharisha wafanyabishara kutojihusisha na vitendo vya rushwa, kupitia dhana ya ufadhili wa gharama za uchaguzi ndani ya Vyama vya Siasa.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU John Mbungo wakati anafungua warsha ya wadau wa uchaguzi, kujadili namna ya kudhibiti vitendo vya rushwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa October 2020.
“Mara nyingi chanzo kikuu cha rushwa katika uchaguzi ni gharama za uchaguzi, jambo hili husababisha wagombea au watia nia kutumia ushawishi pamoja na nguvu ya fedha ili kurubuni wapiga kura wawachague” Brigedia Mbungo
“Mgombea au wagombea wenye uwezo wa kifedha, hutumia kigezo hicho cha fedha kuwarubuni wananchi ili wawachague,” Brigedia Mbungo.