Dunia ina vituko sana unaambiwa hivi nchini Ufaransa ni ruksa kwa mtu kufunga ndoa na maiti sharti tu apate ruhusa kutoka Rais na Waziri wa Sheria wa nchi hiyo.
Desturi hii chimbuko lake limetoka wakati wa vita ya kwanza ya dunia ambapo wachumba na wapenzi wa wanajeshi waliouawa kwenye vita hiyo walifanya utamaduni huo kuonesha upendo wao wa dhati kwa wapenzi wao waliouawa.
Ili mtu aruhusiwe kufunga ndoa hii anatakiwa kuthibitisha kwa kuleta ushahidi unaoonesha kuwa marehemu alipanga kufunga naye ndoa.
Na wakati wa adhimisho la sherehe ya kufunga ndoa bwana harusi ama bibi harusi atasimama pembeni ya picha ya marehemu na sentensi ile ya ‘Mpaka kifo kitakapotutenganisha’ huondolewa kwenye kiapo, na lile jibu wanalotakiwa kujibu maharusi la ‘Ndio’ husemwa ‘Nilikubali’
TAARIFA YA HABARI: Watu watatu walivyocharangwa na Kisu jumba la FISI