Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo November 21 2016 ameendelea na ziara yake mkoani Dar es salaam ambapo leo ikiwa ni siku ya tatu ameanza katika wilaya ya Temeke. Katika Ziara yake hiyo RC Makonda amekusudia kukutana na wananchi kwa ajili ya ya kujibu kero mbalimbali za wananchi.
Ziara ya leo, RC Makonda alianzia kwenye ofisi za mkuu wa wilaya ya Temeke na kuzungumza na watumishi mbalimbali ambao baadaye aliambatana nao kwenye maeneo mbalimbali ili kukutana na wananchi wa Temeke katika maeneo mbalimbali na kujibu kero zao.
RC Makonda ameendelea na ziara yake ya kujibu kero za wananchi, leo ameanzia hapa ofisi ya mkuu wa Wilaya Temeke #DarMPYA #TEMEKE pic.twitter.com/RxPgMZo9rT
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
'Fedha tunayoitumia kwa mishahara ni nyingi kuliko iliyopangwa kwa ajili ya maendeleo lakini wapo watumishi ni mizigo'-RC Makonda #DarMPYA
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
'Pale mkoani ofisini kwangu nina wasaidizi 120 lakini ambao ninaweza kujivunia ni wanne tu, wengine wote ni mizigo' -RC Makonda #DarMPYA
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
'Watumishi wa umma hatumuwakilishi kikamilifu Rais John Magufuli'- RC Makonda #DarMPYA #TEMEKE
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
'Sitaendelea kuwa na wavivu kwenye mkoa huu, lazima ifike muda kila mkuu wa idara ajulikane anafanya kazi gani'-RC Makonda #DarMPYA #TEMEKE
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
'Watumishi mnapaswa kutoka maofisini kutafuta majawabu ya wananchi wenu, watumishi wengi mmekuwa chanzo cha migogoro'-RC Makonda #DarMPYA
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
'Tutawapunguza watu kazini kwa ajili ya manufaa ya umma' -RC Makonda #DarMPYA #TEMEKE
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
'Tunataka watu wanaofikiri nje ya box, ndugu zangu mambo yanawezekana, tusiseme hakuna bajeti'-RC Makonda #DarMPYA #TEMEKE
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
'Kipindi cha nyuma kiongozi alikuwa akisema jambo anazomewa, hatutaki kurudi nyakati hizo'-RC Makonda #DarMPya
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
'Baada ya wananchi keko DSM kusema kuna askari wanachukua rushwa, wameombwa kwenda kuwabaini ili wachukuliwe hatua #DarMPya
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
'Wafanyabiashara wa keko tabia ya kuvamia maeneo ambayo hayastahili, nikiwabaini nitawashughulikia'-RC Makonda #DarMPYA #Temeke
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
'Rais wetu anataka viwanda, keko furniture mna jina kubwa, jipangeni vizuri tutengeneze mfumo mzuri'-RC Makonda #DarMPYA
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
'Nitamuomba Rais Magufuli apige marufuku furniture kutoka nje, tukuze vya kwetu na tuendeleze vya kwetu'-RC Makonda #DarMPYA #KekoTEMEKE
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
ULIKOSA HII YA WANANCHI KIGAMBONI WALIVYOKUWA WAKITAMANI RC MAKONDA ‘AMTUMBUE’ DMO