Mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa amesema Jumatano kwamba mikusanyiko ya sikukuu pamoja na kusambaa kwa virusi maarufu vya hivi karibuni ulimwenguni kulisababisha ongezeko la maambukizi ya COVID-19 mwezi uliopita.
Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema karibu vifo 10,000 viliripotiwa mwezi Disemba, wakati watu waliolazwa hospitali katika mwezi huo waliongezeka kwa asilimia 42 katika nchi takribani 50, hasa za Ulaya na Marekani ambazo zilishirikiana taarifa kama hizo.
“japokuwa vifo 10,000 kwa mwezi ni kidogo sana kuliko wakati janga hili lilipoanza, kiwango hiki cha vifo vinavyoweza kuzuilika hakikubaliki,” mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) aliwaambia waandishi wa habari kutoka makao makuu yake mjini Geneva.
Alisema ni “uhakika” kwamba visa vinaongezeka katika maeneo mengine ambayo hayajaripoti, akitoa wito kwa serikali kuendelea kufuatilia na kutoa fursa ya kuendelea kupata matibabu na chanjo.
Tedros Adhanom Ghebreyesus alitoa wito kwa serikali kuendelea kufuatilia kesi hizo na kutoa fursa ya kuendelea kupata matibabu na chanjo.