Mgahawa maarufu jijini Dar es Salaam, Samaki Samaki, unajiandaa kusherehekea kilele cha miaka 17 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007, sambamba na mgahawa wake mwenza, KUKUKUKU, ambao nao unakaribia kutimiza miaka minne tangu kuanzishwa mwaka 2020. Maadhimisho haya yanatarajiwa kufanyika kwa shangwe kubwa, yakitarajiwa kuleta burudani tele kwa wakazi wa jiji hilo na wageni wengine.
Kwa mujibu wa mmoja ya wafanyakazi wa migahawa hiyo,THE FIXER QUEEN,amesema kuwa tukio hilo la kipekee litatimua vumbi Mlimani City, ambapo wageni watapata fursa ya kushuhudia burudani za aina mbalimbali zitakazowapa furaha na kumbukumbu zisizosahauli
THE FIXER QUEEN ameongeza kuwa sherehe hizo zitakuwa na matukio maalum ya muziki, michezo ya kusisimua, yote yakilenga kuonyesha shukrani kwa wateja waliounga mkono migahawa hiyo tangu kuanzishwa kwake. “Huu ni wakati wa kuadhimisha mafanikio yetu na kusherehekea pamoja na wateja wetu ambao wamekuwa nasi kwa muda mrefu,” alieleza.
Mgahawa wa Samaki Samaki umekuwa kivutio kikubwa jijini Dar es Salaam kutokana na umaarufu wake wa kuandaa vyakula vya baharini vya hali ya juu, huku KUKUKUKU ukitoa ladha maalum za vyakula vya kuku. Maadhimisho hayo yanatazamiwa kuvutia watu wengi na kufungua ukurasa mpya katika safari ya migahawa hiyo miwili ya kisasa.