Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewaagiza maafisa Utamaduni kote nchini kuhakikisha kuwa wanasajili kumbi zote za starehe na kuhakikisha kumbi hizo zinakidhi vigezo vyote kwa mujibu wa kanuni za baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kabla ya Novemba 30, 2023 na kuwasilisha taarifa kwa Katibu Mkuu.
Mhe. Ndumbaro ametoa maagizo hayo Oktoba 11, 2023 jijini Dar es Salaam alipofanya ziara Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo amesisitiza Wasanii wajisajili na kusajili kazi zao kama Sheria inavyoelekeza.
“Katika eneo hili, namuelekeza Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwinjuma kulisimamia kikamilifu na kuchukua hatua kwa wale ambao watakua hawajafanya hivyo, siku hizi Usajili unafanyika kwa njia ya mtandao kwenye mfumo wa AMIS, hii inasaidia kutambua wasanii wetu walipo na aina ya Sanaa wanayofanya.
Aidha, Mhe. Ndumbaro amesema Tuzo za Muziki Tanzania maarufu kama Tanzania Music Awards (TMA) zitaboreshwa na kuwa za kisasa na Kimataifa ambapo tayari Kamati ya kuhakikisha hayo yanafanyika imeundwa na itazinduliwa Oktoba 16, 2023.
Katika hatua nyingine Mhe. Ndumbaro ametoa ufafanuzi kuhusu kufungiwa kwa Bondia Hassan Mwakinyo ambapo amesema Wizara, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC) watakaa pamoja kupitia adhabu hiyo na kama itakua sahihi Bondia huyo ataitumikia