Baada ya Chama cha Act wazalendo Zanzibar kufungua rasmini zoezi la uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi mbali mbali za Kitaifa kichama tarehe Kumi na nne mwezi wa Pili , leo hii Wagombea hao wameendelea Kujitokeza na kufunguliwa Milango Makao Makuu ya Chama Hicho Vuga Visiwani Zanzibar kwa zoezi la Kuchukua fomu
Mchakato huo umefunguliwa Rasmini na unatarajiwa kufungwa kwa zoezi hilo Tarehe ishirini na nne mwezi wa Huu Pili ambapo watangaza nia hao wamekumbushwa kurudisha Fomu hizo kwa wakati Uliopangwa
Kwa Upande wake Ndugu Yunus Abrahman ambae aliejitokeza Makao makuu hayo ya Act wazalendo kwa Mchakato wa Kuchukua Fomu ya Kugombea nafasi ya Halmashauri Ngome ya Vijana Act Wazalendo Zanzibar amesema lengo la kuchukua Fomu hiyo ni kuendelea kuwahamasisha vijana na Kuwafanya waonekane wenye maamuzi katika ngazi mbali mbali za Chama
Nae ndugu Khadija amour ambae ni mgombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya chama cha Act wazalendo Kada ya Pemba amesema ataendelea Kujitoa na Kuhakikisha chama hicho kinashinda nafasi zote licha ya Changamoto zilizomkumba wakati akigombea nafasi ya Ubunge na Kukosa Jimbo la Wawi Pemba na kupatwa na Changamoto mbali mbali ikiwemo za kupigwa Bado ata ataendela kutetea nafasi mbali mbali
Vilevile Naibu Katibu wa Kampeni za Chaguzi ACT Wazalendo Zanzibar Muhene Said Rashid amesema mchakato huo umeanza Tarehe Kumi na Nne na unatarajiwa Kufungwa Tarehe Ishirini na nne na amewataka Wagombea hao kuzingatia wakati wa Kurudishwa Fomu hizo kinyume na tarehe hiyo ugombea wake wa nafasi utakua ni Batil.