Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA akiwa kwenye kampeni Zanzibar amesema Maalim Seif wa ACT-Wazalendo ndio sauti ya wazanzibari kwa miaka 35, hajawahi kubadilisha msimamo wake juu ya kuitetea Zanzibar, kuna kila sababu ya kuungwa mkono kwa msimamo wake.
“Kumuunga Maalim Seif mkono na ACT sio kuwasaliti watu wetu, ni kutambua ukweli ulioko wazi kwa kila mtu kwamba, hawa ni chama kinachoweza kuiondoa CCM madarakani” Tundu Lissu
“Mtu pekee na Kiongozi pekee wa Chama cha Upinzani mwenye nguvu na uwezo wa kuishinda CCM Zanzibar, ni Maalim Seif na Chama cha ACT-Wazalendo, lazima sisi wa huku Bara tumuunge mkono” Tundu Lissu