Moja ya stori iliyomake headlines hivi karibuni ni hii ya kuhusu mkulima wa kijiji cha Dodoma Isanga kata ya Masanze wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro aliyechomwa mkuki mdomoni na ukatokea shingoni kwa kikilichoelezwa ni mgogoro wa ardhi ambapo madaktari walifanikiwa kuokoa maisha yake baada ya kumfanyia upasuaji.
Leo December 29 2016, Waziri wa ardhi, William Lukuvi, mkuu mkoa wa Morogoro, Dkt. Steven Kebwe wakati wakifungua semina juu ya jukumu la vyombo vya habari katika kutoa elimu juu ya masuala ya ardhi wamezungumzia kuhusu mkulima huyo aliyechomwa mkuki.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Waziri Lukuvi amesema tukio hilo si mgogoro wa ardhi bali ni uhalifu na vyombo vya dola vimeshachukua hatua. Aidha mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe amesema watu 13 wameshakamatwa wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo. Bonyeza play hapa chini kutazama.
VIDEO: Mpaka 2015 kulikua na Watu Milioni moja laki 4 wanaoishi na VVU Tanzania, Bonyeza play hapa chini