The Blues tayari wamewasilisha ofa tatu, huku ofa ya hivi punde inayoaminika kuwa karibu pauni milioni 80 kwa jumla, ilikataliwa na Seagulls kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ecuador.
Brighton wanadaiwa kushikilia pauni milioni 100 huku Chelsea wakifanya kila wawezalo kupunguza bei hiyomasharti ya kibinafsi tayari yamekubaliwa kwa maneno, bila chochote kusainiwa bado.
Tatizo kubwa limekuwa ni tathmini tofauti za klabu hizo mbili za mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, lakini ikiwa imesalia chini ya mwezi mmoja kabla ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi kukamilika, kunahitajika suluhu kwa njia moja au nyingine haraka sana.
Kuelekea mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya Uingereza Jumapili dhidi ya Liverpool, mkufunzi wa Chelsea Mauricio Pochettino hana chaguo la kiungo.
Muargentina huyo kwa sasa ana Enzo Fernandez, Conor Gallagher, Andrey Santos, Carney Chukwuemeka, Lesley Ugochukwu na Cesare Casadei. Wawili wa mwisho kati ya hao Ugochukwu na Casadei -wanaweza kukopeshwa kwa ajili ya kampeni ijayo, hata hivyo, kuwaacha Blues pungufu.