Mama mzazi wa mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford, amesema kuna wakati alilazimika kulala njaa ilimradi watoto wake wapate chakula.
Kwa mujibu wa Mama Rashford, Melanie Maynard, waliishi maisha magumu yaliyolazimisha awe anafanya kazi katika maeneo matatu tofauti.
“Nilikuwa nafanya kazi tu na kama si hivyo, basi tungekufa njaa, yalikuwa maisha magumu kidogo” Mama Rashford
Ushuhuda wake unakuja wakati Rashford akiwa ‘bize’ na kampeni zake za kutoa misaada ya vyakula kwa watu wenye mahitaji, wakiwamo watoto.