Meneja Uhusiano wa TANESCO Johari Kachwamba, amesema kuwa uwepo wa kunguru ndiyo chanzo kikubwa cha umeme kukatika mara kwa mara katika Wilaya ya Kinondoni Jijini DSM, kwani Kunguru hao wanachangia kuharibu miundombinu hususani nyaya za umeme.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 5, 2021 “Kinondoni tuna tatizo la kunguru kuathiri sana miundombinu yetu, tunatumia nyaya zenye magamba ya ‘silver’ ambazo zinaathirika sana na katika kutatua hili tumeanza kubadilisha nyaya, tunazoziweka sasa hivi hazitakuwa zinaathirika kiurahisi na kunguru”
‘Ni tatizo linalotokea mara kwa mara na si sehemu ya tatizo kubwa ambalo tunaweza kusema watu wa Kinondoni wanashindwa kufanya kazi zao” Johari
“Uwepo wa kunguru wengi wanaonyanyua nyaya kwenye madampo ya taka na kwenye viwanda vya nyaya vilivyoko maeneo mengi ya Kinondoni ikiwepo machinjio, inafanya kunguru kutua kwenye nyaya za umeme wa msongo mkubwa (33KV na 11KV) na kusababisha milipuko kati ya waya na waya, pia wakittua kwenye ‘Transformer’ husababisha milipuko na hizo nyaya wanazobeba kwa ajili ya kutengeneza viota vyao” Johari