Serikali ya mpito nchini Niger imetangaza kuwa msafara wa kwanza wa wanajeshi wa Ufaransa walioko nchini humo utaanza kuondoka Jumanne hii, ya Oktoba 10.
Akiisoma taarifa kwa vyombo vya habari jumatatu jioni kupitia televisheni inayomilikiwa na utawala wa kijeshi nchini humo, mkuu wa kamati iliyoundwa ili kufuatilia kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa nchini Niger, Kanali-Meja Mamane Sani Kiaou, ni kuwa ratiba ya kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa imeamuliwa” kwa makubaliano na pande zote mbili.
Hata hivyo Kwa sasa, jeshi la Ufaransa halijajibu tangazo hili.Huku mamlaka jijini Niamey ikisema kuwa shughuli za kuondoka kwa jeshi hilo itafanyika kuanzia jumanne hii ambapo vikosi vya ulinzi na usalama vya Niger vimewekwa tayari kuwasindikiza wanajeshi hao wa Ufaransa watakapoanza kuondoka.