Matukio ya watu kupigwa risasi yamekuwa yakichukuwa headlines kubwa hasa kwa Dar es salaam lakini sio mwajiri kumpiga risasi mfanyakazi wake, Sasa hii imekuwa tofauti kidogo ambapo Jumanne ya wiki hii ililipotiwa tukio la Mwajiri kumpiga risasi mfanyakazi wake baada ya kusababishia Kampuni ya Tripple A KTM, hasara ya dola za Kimarekani 200 sawa na 400,000 za kitanzania na lita 700 za mafuta baada ya kufika nchini akitokea Congo.
Akiongea na ripota wa millardayo.com Naibu katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa madereva (TADWU) Rashidi Salehe…’Niliongea na marehemu nusu saa kabla ya kifo chake akinitaarifu kuwa anashoti ya lita sabini za mafuta na anaupungufu wa dola mia mbili (200) ambazo alizitoa kama sehemu ya faini ya mizani upande wa Zambia sehemu ya Kapilimposhi, kwahiyo alikuwa akinitaarifu huwenda anaweza akapelekwa Chang’ombe kituo cha Polisi ambacho amekuwa akikitumia sana mmiliki kuwapeleka madereva akanimbia kwamba niwe na angalizo huwenda akawekwa ndani,dakika kumi baadae nilipigiawa simu na mwanachama wetu mbaye ni deverva wa kampuni hiyo kwamba David amepigwa risasi na ameanguka chini’>>>Rashidi Salehe Naibu Katibu TADWU
‘Sasa leo tunataka kuona kupitia kilio chetu cha kudai maslahi yetu na hatimaye mauaji serikali inatoa tamko gani? lakini sisi kama vyama vya wafanyakazi tumelaani tukio hili na tunasema kwamba hatua zichukuliwe haraka iwezekanavyo, tumejitahidi sana kuwatuliza madreva watulie katika kipindi hiki vinginevyo hatua ilikuwa mbaya zaidi juu ya magari ya mmiliki huyo yaliyokuwa boda na Dar es salaamu kwa sababu amekuwa akiyafanya mambo haya marakwamara suala la kupiga bastola kupiga mpaka ilifikia hatua Kova alidhibitisha kwamba bastola yake ilikamatwa kwa mara ya kwanza’>>> Rashidi – TADWU
‘Endapo kesi hii itasimama maahakamani kila siku ya mahakama tutakuwa tunasitisha usafiri nchi nzima kama sehemu ya kilio chetu juu ya mauaji ya kinyama yaliofanyika kwa dereva mwenzetu Bwana David Kilangula’>>>Rashidi- TADWU
Bonyeza Play kumsikiliza katibu wa chama cha wafanyakazi madereva TADWU.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE