Takribani kila nchi ulimwenguni inakumbana na baadhi ya visa vya udhibiti wa mtandao kinachotofautisha nchi dhidi ya nchi nyingine ni tovuti na viunzi gani vimefungwa, na athari ya kufungwa huko.
Wakati wa kura na maandamano ulimwenguni, serikali kila mara uagiza kufungwa kwa mitandao ya kijamii inayotumika sana kama vile WhatsApp,X na Facebook .
Katika nchi nyingi, serikali pia uagiza kufungwa kwa vyombo vya habari huru, tovuti za makundi madogo, na idadi nyinginezo mashirika ya mitandaoni.
Ni vipi tunaweza kuwa na uangalizi wa udhibiti wa mtandaoni ulimwenguni ?
Utafiti unaonyesha kuwa kuzimwa kwa mitandao kunaathiri makumi ya mamilioni ya watu duniani kote kwa namna mbalimbali.
Maafisa wa serikali wana uwezo wa kuzima mtandao kwa kutoa agizo kwa watoa huduma hiyo kuzima intaneti katika baadhi ya maeneo au mara nyingine, huwa wanafungia upatikanaji wa huduma za tovuti kwenye maeneo mbalimbali.
Makundi ya haki za binadamu wanaona kuwa hiyo ni mbinu ambayo serikali inatumia kuwanyima watu haki zao katia maeneo mbalimbali duniani.
Maranyingi serikali inapotoa agizo la kuzimwa kwa mitandao huwa ni kuhakikisha kuwa kuna usalama na kuzuia kwa taarifa ghushi lakini wakosoaji wanasema kuwa kuzimwa kwa taarifa mtandaoni huwa kuna athiri shughui nyingi muhimu.
Shirika la Zaina Foundation kupitia mafunzo yake limetoa mambo muhimu kwa waandishi wa habari kuhusu zana mbalimbali kuhusiana na kuzimwa kwa mtandao hasa kujifunza jinsi ya kupima udhibiti wa mtandao kwa kutumia zana za OONI.
Kipimo cha OONI ni programu ya kompyuta inayopatikana bila malipo iliyoundwa na Shirika la Ufuatiliaji wa Kuingiliwa kwa Mtandao yaani Open Observatory of Network Interference (OONI) ambacho kinaweza kutumiwa kutathmini viwango vya kuminywa kwa uhuru wa habari na unaweza kupakua kipengele hiki kwenye simu yako
Kutumia zana data za OONI katika taarifa za kiuandishi kunaweza kuongeza ubora katika taarifa za mwandishi yeyote kwa kurejea data za vipimo vya udhibiti kama ushahidi wa matukio ya udhibiti wa mtandao.
Katika tafiti mbalimbali OONI inatoa programu ya bure, mbinu, na data za wazi ambazo mwandishi yeyote anaweza kuzitumia kama sehemu ya tafiti za kuzimwa kwa mtandao.
Mtu anapotumia kipengele cha OONI, hufanya majaribio kadhaa ili kubaini kiasi cha kuminywa kwa uhuru wa habari kwenye mitandao anayotumia. Kipengele cha OONI hupima vitu vifuatavyo:
Tovuti zilizo zuiliwa..
Kufungwa kwa zana za kusaidia kukwepa udhibiti wa matumizi ya mitandao Tovuti inaweza kuzuiliwa pale ambapo juhudi makusudi zinafanywa kukuzuia kuitumia au unaelekezwa kwenye tovuti ambayo siyo au unashindwa kuingia kwenye tovuti unayotaka kutumia.
2.Utendakazi wa spidi ya mtandao
Unaweza kuangalia iwapo Mtoa Huduma zako za Intaneti (ISP) anakuzuia usitumie app za kutuma ujumbe za WhatsApp, Facebook Messenger, Telegram.
Kwa kutumia OONI Probe, unaweza kuangalia iwapo app za mitandao ya jamii (kama vile WhatsApp na Facebook Messenger) imezuiwa kwenye mitandao yake. Ukitaka kujua kama mtandao mahususi umezuiwa, unaweza kuufanyia majaribio kupitia kitufe cha “Choose websites” kinachopatikana kwenye kadi ya Tovuti hiyo ya app OONI Probe.
Utetezi huleta ufahamu wa madhara yanayosababishwa na kuzimwa kwa intaneti na inaweza kusaidia katika kulinda haki za watu kupitia kushiriki maelezo kuhusu jinsi ya kushughulikia kuzima kwa mtandao na kuangazia zaidi hatua ambazo watu wanaweza kuchukua ili kujiandaa kwa kuzima kwa mtandao.