Takriban watu saba hawajulikani walipo kufuatia bwawa la Nova Kakhovka kuporomoka siku ya Jumanne, meya wa mji huo aliyeteuliwa na Moscow aliliambia shirika la habari la Urusi RIA Novosti siku ya Jumatano.
Wakati huohuo Ukraine, inasema imewahamisha zaidi ya watu 1,500 kutoka maeneo ya Kherson yanayodhibitiwa na mafuriko ya Ukraine.
Mamlaka ziliongeza kwenye chapisho kwenye Telegram kwamba “makazi 20 kwenye ukingo wa magharibi wa Mto Dnipro na zaidi ya nyumba 1,900 zilifurika katika eneo la Kherson.
Zaidi ya saa 24 baada ya uvunjaji wa bwawa la Nova Kakhovka, shughuli ya utafutaji na uokoaji huko Kherson bado inaendelea.
Mamlaka na watu waliojitolea wanaendelea kutumia boti za mbao na boti za mpira kuwahamisha watu – na idadi kubwa ya paka na mbwa – ambao waliachwa wakiwa wamekwama huku kiwango cha maji kikiendelea kupanda usiku kucha.
Wamekuwa wakifanya kazi bila kuchoka tangu jiji lilipoanza kufurika na sasa, wamechoka na kuzidiwa, ni sehemu kubwa ya janga hili.
Watu wanaotoka kwenye boti wanaonekana kupata mstuko kutokana na shida hiyo wengine wakiangua kilio walipofika nchi kavu huku wanyama wakionekana katika dhiki. Vilio vya mara kwa mara na vifijo vinasikika katika eneo la tukio huku shughuli zikiendelea.
Baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa yakifikiwa kwa miguu siku ya Jumanne sasa yako chini ya maji – katika baadhi ya maeneo, maji yana kina cha hadi mita nne (futi 13). Hata hivyo, kuna hisia kutoka kwa mamlaka kwamba viwango vya maji, ingawa bado vinaongezeka, sasa vinafanya hivyo kwa kasi ndogo.
Wakati mzozo wa kibinadamu unaendelea kufichuliwa mbele ya macho yetu, vita viko kila wakati na Kherson inasalia kuwa jiji la mstari wa mbele.