Taarifa zilizoenea mitandaoni saa chache zilizopita, zinahusiana na tukio la kurushiana risasi baina ya aliyekuwa Naibu Waziri wa zamani wa Afya na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Dk. Lucy Nkya na mtoto wake ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Morogoro Jonas Nkya.
Tukio hilo ambalo limetokea leo Morogoro baina ya wanafamilia hao, limehusishwa na ugomvi wa kifamilia jambo ambalo limeamsha hisia tofauti.
Akizungumza na waandishi wa habari Morogoro, Jonas Nkya amekanusha taarifa za kurushiana risasi na kueleza kuwa tukio hilo ni tukio la bahati mbaya baada ya bunduki yake kudondoka na kupelekea risasi mbili kufyatuka.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo, Jonas amesema, “.. silaha inakaa kiunoni, nakwenda kwenye gari nashuka pale ofisini pisto hii imeanguka imejipiga risasi mbili nje ya ofisi. Sasa nadhani majirani wakaogopa sijui mi sielewi, lakini kuna watu wanaishi pale. Sasa ndio ikafika hapo wakaja Polisi of course na nini.. tumejaribu kuwaeleza.. ndio hicho kilichotokea. Lakini mimi sijui.. wala sikujua kama mama yangu yuko ndani kwa sababu pale ofisini nimekwenda kufuata gari .”–Jonas
“.. Na ndio maana nasema kama mkipata muda na nyie mnaweza kwenda kumuuliza yule mama je tumegombana.. je kuna kitu kama hicho.. hiyo ndio habari iko hivyo.. hakuna ukweli kwenye hilo..”–Jonas
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook