Ni vile vitu ambavyo inawezakana unafianya mara kwa mara au umeona wengine wakivifanya kila siku bila kujua madhara yake, mimi mwenyewe sikuwa nafahamu kwamba kutafuna bazoka ‘bigijii’ wakati ukiwa na njaa ni hatari kwa afya yako.
Kwenye mahojiano na DW Kiswahili, Dr. Sizya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili amesema kutafuta bigijii wakati ukiwa na njaa ni hatari na inaweza kukusababishia kuumwa vidonda vya tumbo, Wanasayansi wamethibitisha.
“Kutafuna ‘bigijii’ ukiwa na njaa kunaleta vidonda vya tumbo, tumbo hujiandaa likijua ni chakula kinakuja hivyo linatengeneza acid ili kumeng’enya chakula, sasa kwasababu sio chakula… hizo acid zinakwenda kukwangua kuta za tumbo na kukusababishia vidonda vya tumbo” – Dr. Sizya
.