Paroko wa Kanisa la Katoliki Parokia ya Karatu Mission, Padri Pamphili Nada ameuwa kwa kupigwa na kitu kizito na Mtu anayedhaniwa kuwa na matatizo ya akili aliyeingia Kanisani kwa nguvu usiku na kulazimisha kuombewa na padri huyo.
Bernard Clemence ambaye ni Katibu Msaidizi katika Parokia ya Karatu Mjini amesema Mtu huyo aliingia kanisani hapo majira ya saa nne na nusu usiku akazuiwa na Mlinzi na kuondoka lakini alirudi tena baadaye saa nane usiku na kuzozana na Mlinzi kitendo kilichofanya Padri huyo kutoka na kukubali kumuombea ambapo walipoingia Kanisani Mtu huyo alichukua chuma ya kuzuia mlango na kuanza kumshambulia.
“Kuna chuma ya kuzuia mlango Padri alivyogeuka Jamaa akachukua chuma inavyosemekana akampiga kisogoni, ata yeye alifariki watu walikuwa na hasira na walivyoona damu imetapakaa wakamuunganishia hapo” ameeleza Benard.