Tumeshazoea kuona nchi kubwa ndio zimekuwa zikiandika rekodi za kuzalisha vinywaji vikubwa vikiwemo Henessy, Jameson, Grants, Moet na nyinginezo.
Sasa leo Julai 11, 2023 nakukutanisha na kijana wa kitanzania, Amour Shamte ambae ametuletea bidhaa yake mpya iitwayo Johari Gin.
Kinywaji pekee chenye Gin tofauti na ladhaa yake hautakiwi kupewa hadithi, hapa nakusogezea alichozungumza Amour Shamte hizi ni nukuu zake.
‘Kwanza ningependa kuchukua nafasi hii kuwashukuru millardayo.com & Ayo TV mmekuwa na Mchango mkubwa kwangu kuanzia tangu enzi za Maison Club na leo hii ninamiliki kinywaji kiitwacho Johari Gian’- Mmiliki wa Kinywaji cha Johari Gin, Amour Shamte
‘Johari Gian ni Kinywaji kipya ambacho kina mwezi tangu nikizindue na wazo hili lilinichukua almost miaka miwili iliyopita kwahiyo sio kitu ambacho nimetoka tu usingizi jana nina kiwanda kabisa na kinafanya uzalishaji’- Mmiliki wa Kinywaji cha Johari Gin, Amour Shamte
‘Uandaaji wa Kinywaji hiki natumia nafaka za hapa hapa Tanzania sehemu tofauti tofauti ikiwemo Zanzibar, Morogoro, Iringa na katika kuandaa haichukui muda mwingine kwani Mashine inayotumika kutengeneza hiki kinywaji hiki kinauwezo wa kutoa chupa zisizopungua mia 800 kwa siku’- Mmiliki wa Kinywaji cha Johari Gin, Amour Shamte
‘Na Mtambo ama Mashine hii nimeinunua nchini Ujerumani ambaYo ufanyaji kazi wake ni tofauti kabisa lakini nina mpango wa kuleta mashine zingine ili uzalishaji uwe mwingine zaidi kwani nahitaji kuzalisha kwa siku zaidi ya chupa 2500’- Mmiliki wa Kinywaji cha Johari Gin, Amour Shamte
‘Na katika hatua hii niliona nitoe ajira pia kwa wafanyakazi wa kigeni ili bidhaa inayozalishwa iwe bora zaidi hivyo nina raia wa kigeni ambao wapo katika uzalishaji huu wakisaidiana na watanzania wengine juu ya kuchakata nafaka hizo ambazo zinatumika kutoa kitu halisi’- Mmiliki wa Kinywaji cha Johari Gin, Amour Shamte
‘Na katika kuunga juhudi za Serikali uwepo wa kiwanda na nimetoa ajira kwa Vijana wasiopungua 15 ambao wanahakikisha uandaaji unakuwa kwa haraka ila kadri siku zinavyozidi kwenda nitahitaji watu hata 100 wakiwemo madereva watakaokuwa wanasambaza mikoani kwahiyo hii ni project endelevu na inaendelea kuzalishwa kila siku’- Mmiliki wa Kinywaji cha Johari Gin, Amour Shamte
View this post on Instagram
‘Spirit ya kinywaji hiki si kali hata test yake ni ladhaa ya kitofauti kabisa na kwasasa inapatikana Dar es Salaam, Moshi na Arusha tunawakala wetu wapo katika hiyo mikoani miwili ila siku zijazo tutawafikia mikoa mingine hivyo naomba wale wanywe wajaribu kinywaji hiki kipya cha kwangu mimi mtanzania Amour sio kikali na wala hakiumizi kichwa pale unapoamka asubuhi kwani Gin tunayoitumia ni tofauti na zingine ambazo mnywaji amezizoea’- Mmiliki wa Kinywaji cha Johari Gin, Amour Shamte
‘Kwasasa nataka kuhakikisha kwanza Tanzania nzima kinawafikisha na kutoa Elimu halafu ndipo nitaipeleka rasmi East Africa ikiwemo Kenya, Uganda na nchini zinginezo kisha next Worldwide hivyo mipango ipo lakini kwasasa naanza na nyumbani wakitambue kuwa kuna Johari ambayo imeanzishwa na Mtanzania’- Mmiliki wa Kinywaji cha Johari Gin, Amour Shamte
‘Kwanini Wazungu ama mataifa mengine waweze kuzalisha vinywaji vyao na tunakunywa sisi wa ndani kwanini tusiwe wabunifu hivyo ndio maana nimeileta Johari Gin na nina amini hii brand itafika mbali na tutapata raia wa kigeni watakaokuja kushuhudia kila kilichobora’- Mmiliki wa Kinywaji cha Johari Gin, Amour Shamte
‘Kwa Dar inapatikana Sehemu ikiwemo 1245 Lounge, Elements Bar Masaki, Tips Lounge, Uncles Masaki, Tips Kidimbwi Mbezi Beach, Tips Coco Beach na zinginezo’- Mmiliki wa Kinywaji cha Johari Gin, Amour Shamte
‘Na Episode za utambulisho wa kinywaji hiki utakuwa unaambatana na mastaa wakubwa wa Afrika hata nje ya Afrika awe msanii ama Dj’s na wikiendi hii episode yetu itaendelea pale Elements Masaki Dar ambapo usiku huo utashehereshwa na Dj kutokea Afrika Kusini huyu si mwingine ni Tyler ICU mwenye hit song iitwayo Mnike’- Mmiliki wa Kinywaji cha Johari Gin, Amour Shamte
“Naomba Watanzania hususani wanywaji wani support mimi mtazania kuonesha Uzalendo kwani tunaweza kuzalisha pia vya kwetu kupitia Nafaka zetu hakika tunaweza na Johari iko inapatikana katika hizo sehemu nilizozitaji kwa bei nafuu tu’- Mmiliki wa Kinywaji cha Johari Gin, Amour Shamte
Hizi ni baadhi ya Picha ambazo hafla hii ilifanyika siku kadhaa zilipopita kwenye rooftop iliyopo Palm Village Mikocheni, utambulisho wa kinywaji hicho kipya Johari Gin.