Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe alisimama Bungeni kujibu swali la Mbunge wa viti maalum CCM Catherine Magege aliyehoji sababu za Serikali kufungia nyimbo za wasanii baada ya kuziachia na kushindwa kuzuia tatizo hilo kabla.
Waziri Mwakyembe amesema…>>>“Kama Serikali hatuna shida na wasanii wetu, lengo letu ni kulinda maadili, kila taifa lina maadili yake na ndio maana hata wakina Rick Ross na Wizkid wanafungiwa kazi zao, sisi tunalalamika kufungiwa kwa nyimbo mbili? Tutaendelea kuwafungia ili kulinda utamaduni wetu ”
Atakachokifanya Mtoto Anthony akipata Mshahara wake wa kwanza