Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja Rc Ayoub Mohammed Mahamoud amesema baada ya ofisi yake ya mkoa kuwagaiwia chai na mikate ya siagi watumishi wake kumepungua matukio ya watumishi kuzura nyakati za kazi huku akitarajia kueka miundombinu ya simu za ofisi ila watumishi waache simu zao majumbani
Rc ayoub ameyasema hayo baada ya kuhitimisha ziara yake ya kustukiza katika mkoa wa kusini unguja na kuwabaini watumishi 40 wanaochelewa makazini huku akimuagiza Mkurugenzi wa Baraza la Mji kati kusini kuwapa Barua wasimamizi Maafisa Utumishi wenyejukumu la kuwasimamia watendaji kwa kushindwa kuwaonya wachelewaji hao makazini
Ayoub amesema aliamua kufanya ziara hiyo ya kustukiza ili kuwabaini wachelewaji ambapo pia amesema kwa sasa anaridhishwa na utendaji kazi katika ofisi yake kwa sasa anakamlilisha taratibu za mawasiliano ili wafanya kazi hao kutoenda na simu zao makazini kwa atakaehitajika kumpigiwa simu au kupiga simu za ofisini hapo zitatumika