Kama unakumbuka hivi karibuni Rais Magufuli alizindua magari ambayo yatatumika kusambaza dawa na akasisitiza kuwa uwepo wa viwanda vya dawa Tanzania utasaidia kuokoa mamilioni ya pesa ambayo Tanzania hupoteza kwa kununua dawa nje ya nchi kila mwaka.
Baada ya kauli hiyo ya Rais Magufuli kutaka Watanzania kujitokeza kuwekeza kwenye viwanda vya dawa Tanzania, leo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa na Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage wamekutana na wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba na unaambiwa tayari kampuni zaidi ya 30 zimeonyesha utayari