Vifo vitokanavyo na ugonjwa wa Ukimwi vimepungua kwa asilimia 50, kutoka vifo 64,000 kwa mwaka 2010 hadi 32,000 mwaka 2020 huku kiwango cha maambukizi katika jamii kikishuka kutoka 7% mwaka 2003/04 hadi 4.7% mwaka 2016/17.
Mfanikio hayo ni kufuatiwa juhudi za Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambapo wamefanikiwa kudhibiti maambukizi ya VVU na Ukimwi. kwa mujibu wa kiwango cha upimaji wa VVU kimeongezeka kutoka asilimia 61 hadi asilimia 83 ya makisio ya watu wanaoishi na VVU (WAVIU).
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2021.
Waziri Mhagama alieleza kuwa kiwango cha upimaji wa VVU kimeongezeka kutoka asilima 61 ya makisio ya watu wanaoishi na VVU (WAVIU) mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 83 mwaka 2019.
“Serikali kupitia uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan imepiga hatua kubwa katika kudhibiti VVU na Ukimwi nchini,” Waziri Mhagama.