Balozi Getrude Mongella amesema imefikia wakati wa kuachana na matumizi ya nishati ya Kuni na Mkaa badala yake kuanza kutumia Nishati safi ya Kupikia ambayo ni Gesi na Nishati ya bayogasi ili kulinda na kuthamini Afya na Hali za Wanawake.
Balozi Mongella Ameyasema hayo Leo Jijini dar es salaam katika Mjadala wa Kitaifa wa Nishati safi ya Kupikia wakati wa mdahalo wa Mchango wa Wanawake katika Kuhakikisha matumizi ya nishati safi inapigiwa chapuo.
Hata Hivyo, Balozi Mongella amempongeza Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba Kwa kufanikisha Mjadala wa Nishati safi ya Kupikia unaofanyika ili kuleta Mapinduzi Makubwa kwenye matumizi ya nishati muhimu zenye kutunza Hadhi ya Kila mwananchi akisema “Ngoma imepata mchezaji”.