Ni Feb 6, 2024 ambapo kwa mara nyingine tena kampuni ya Asas inayohusika usambazaji na uuzaji wa Maziwa Tanzania Usiku huu imetunukiwa tuzo ya heshima kwa viwango vya Ubora wa bidhaa na huduma kutoka Superbrand East Africa Choice 2022/2024.
Shughuli za utoaji wa tuzo hizo zimefanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
Aidha Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Abdallah Asas amewashukuru Watanzania na wadau kuendelea kuiamini kampuni hiyo hususani kwenye usambazaji na uuzaji wa Maziwa.
‘Kipekee nichukue nafasi hii kuwashukuru waandaji wa tuzo hizi za Superbrand, kushinda tuzo hii ni ishara tosha ya juhudi za Uzalishaji, Usambazaji na uuzaji wa Maziwa yetu nchini kuendelea kuwa bidhaa muhimu katika jamii’- Abdallah Asas Mkurugenzi wa Kampuni ya Uuzaji na Usambazaji
‘Kila mwaka maelfu ya bidhaa kutoka sekta tofauti zinaamuliwa dhidi ya ya vigezo vitatu vya muhimu vya Superbrand: ubora, kuaminika na utofauti. Kufikia hali ya kutunukiwa hadhi ya Superbrands ina maana hadhi ya bidhaa husika inaongezeka na huwahakikishia watumiaji na wauzaji kuwa wananunua bidhaa iliyobora kabisa’- Abdallah Asas Mkurugenzi wa Kampuni ya Uuzaji na Usambazaji
‘Tuzo hii ina maana kubwa kwa wateja wetu kwa kuendelea kuiamini ASAS kwa zaidi ya miaka 80.Tunawashukuru sana wateja wetu ASAS tutaendelea kuwapatia huduma za viwango vya ubora wa hali ya juu’- Abdallah Asas Mkurugenzi wa Kampuni ya Uuzaji na Usambazaji
Hizi ni picha mbalimbali kutoka kwenye hafla hiyo ambayo imefanyika Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam, tazama mwakilishi wa ASAS alivyoipokea tuzo hiyo ya Superbrand.