Katika hali ya kihistoria nchini Mexico, Claudia Sheinbaum anatarajiwa kuwa rais wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa kishindo katika kura za urais nchini humo.
Mwanasayansi wa hali ya hewa na meya wa zamani wa jiji la Mexico, Sheinbaum alinufaika na mshauri wake na rais anayemaliza muda wake Andres Manuel Lopez Obrador u kupata 58.3% hadi 60.7% ya kura kama inavyoonyeshwa katika sampuli ya haraka ya mamlaka ya uchaguzi ya nchi hiyo.
Hii ndiyo asilimia kubwa zaidi ya kura katika historia ya kidemokrasia ya Mexico.
Zaidi ya hayo, muungano unaotawala pia ulikuwa kwenye njia ya kupata thuluthi mbili ya wengi zaidi katika mabunge yote mawili ya Congress kuwaruhusu kupitisha mageuzi ya kikatiba bila kuungwa mkono na upinzani, kulingana na anuwai ya matokeo yaliyotolewa na mamlaka ya uchaguzi.
“Kwa mara ya kwanza katika miaka 200 ya jamhuri nitakuwa rais wa kwanza mwanamke wa Mexico,” Sheinbaum aliwaambia wafuasi wake kwa shangwe kubwa za “rais, rais”.
Ushindi wake ni hatua kubwa kwa Mexico, nchi inayojulikana kwa kuwa nchi ya pili kwa ukubwa duniani ya Wakatoliki wa Roma, ambayo kwa miaka mingi ilisukuma maadili na majukumu ya kitamaduni zaidi kwa wanawake.
Sheinbaum ndiye mwanamke wa kwanza kushinda katika uchaguzi mkuu nchini Marekani, Mexico au Kanada.