Kama ulikuja Dar es Salaam miaka kumi iliyopita na ukirudi kwasasa basi lazima ukute mabadiliko makubwa yaliyofanywa katika Sekta mbalimbali kuanzia Barabara, Majengo na mengineyo.
Ukiacha uboreshwaji uliofanywa kwenye sekta mbalimbali kingine ambacho kimenivutia ambacho huenda utapendezwa nacho.
Ni kuwepo na eneo jipya linalofahamika kwa jina la 1245 ambalo ukutanisha watu mbalimbali wakiwemo mastaa kwaajili ya kuburudika huku wakiwa na Headphone ambayo mdau usikiliza nyimbo zinachezwa na Ma DJ’s mbalimbali akiwemo Dj Nyosk, Dj Jazzy, Dj Joozey.
Eneo tangu lizinduliwa lina miezi kadhaa na hivi karibuni kumekuwa na sintofahamu kutokana na sheria zao mpya walizoweka kwa wateja wao.
Kwasasa 1245 wameweka sheria za Mavazi ambayo kwa mteja wao atakaefika katika eneo lao hatoweza kuingia kupata huduma yao.
Akizungumza na Millardayo.com msemaji wa 1245 ambae hakutaka jina lake litajwe alisema..’Unajua kitu utofauti wetu sisi na sehemu pengine ni ubora wa kazi zetu kuanzia Muziki, huduma inayotolewa na mambo mengi tu its all about Services’-
‘Na kwa hii miezi kadhaa tangu kuifungua hii 1245 mengi tumejifunza mengi na maoni pia tumepokea kwa wadau kuwa nini kiwepo ama nini kiondolewe nia na dhumuni wateja wetu wafurahie huduma zetu’
‘Sasa miongoni mwa maoni ambayo tumekuwa na tumelitekeleza ni hili kuhusu mavazi na mteja anaekuja kwetu 1245 kama atakuwa na Slides, Open Back sandals, Crocs, Flipflops, Hoodie, ama Kaushi (Vest for men), Face Masks hatoruhusiwa kuingia katika eneo letu’-
‘Mteja akizingatia aina ya mavazi ambayo tumeyakataza basi huyo ataweza kuhudumiwa na kuona kila kilichobora katika eneo letu, narudia tena hatuna na watu wasituchukulie vibaya lazima tufuate Sheria inavyosema’
‘Milango iko wazi karibuni na leo Jumamosi tuna wakali kutoka Afrika Kusini hawa si wengine ni 2wobunnies ambao watatua masaa yasiyopungua manne kuwaburudisha watanzania ama wapenzi wa nyimbo za Amapiano karibuni’