Diwani wa Kata ya Bomambuzi Manispaa ya Moshi Juma Raibu ameingilia kati sakata la Bibi Elizabeth anayetaka kuondolewa katika kiwanja chake alichoishi hapo miaka 70 toka enzi za Mwalimu Nyerere.
Akizungumza na Bibi huyo Diwani Juma Raibu amemtoa hofu na kumuahidi suala lake atalifikisha sehemu husika na Bibi huyo ataendelea kubaki eneo hilo kwa amani.
Aidha Diwani huyo ameiomba TAKUKURU kulichunguza jambo hilo kutokana na ubababaishaji anaofanyiwa Bibi.