Tafiti mbalimbali zimeendelea kufanywa duniani kote, hivi karibuni CAF World Giving Index, kwenye ripoti yao ya mwaka 2016 wamefuatilia kiwango cha ukarimu duniani kote.
Unaambiwa matokeo ya utafiti huo yanaweza kukushangaza kidogo kwani nchi ambazo watu wake wameishi kwenye mazingira ya hatari zaidi ndio zimetajwa kuongoza kwa kuwa wema na msaada kwa wageni.
Nchi hizo ni Iraq na Libya, wananchi wake wamevumilia miaka mingi ya vita, mashambulizi ya kigaidi na machafuko kwa ujumla.
Unaambiwa kuwa hata kabla ya vita kuibuka nchi zote mbili zimekuwa na utamaduni wenye nguvu wa kusaidia jamii. Kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchi ya Libya, 72% ya watu walisema waliwasaidia wageni, leo idadi hiyo inasimama kwenye 79%.
Nimekuwekea Hapa Top 10 ya nchi ambazo watu wake wamekuwa wema kwa wageni
VIDEO: Lissu alivyoeleza mipango ya CHADEMA kwenye kesi za mbunge Lema, Bonyeza play hapa chini