Leo January 02 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemaliza ziara yake ya siku mbili Mkoani Kagera kwa kuwatembelea baadhi ya wananchi walioathiriwa na tetemeko la ardhi pamoja na kukagua baadhi ya miundombinu iliyoathiriwa na tetemeko hilo.
Mara baada ya ukaguzi huo Rais Dkt. Magufuli akazungumza na wananchi wa Mkoa huo wa Kagera katika viwanja vya shule ya sekondari ya Ihungo na kuagiza kuvunjwa kwa kamati ya maafa ya mkoa huo iliyokuwa ikiratibu utoaji wa misaada na kufanya tathmini ya athari ya tetemeko hilo.
Aidha Dkt Magufuli amewataka wote walioahidi kuchangia katika kamati ya tetemeko la ardhi ya mkoa wa Kagera ambao bado hawajatekeleza ahadi zao ambazo ni jumla ya BIL 4.5 wakamilishe ahadi hizo ili ziweze kumalizia miundombinu ya Serikali iliyoathiriwa na tetemeko hilo.
Ameongeza kuwa wale wote wanaoendelea kuguswa kusaidia wapeleke michango yao moja kwa moja kwa wananchi badala ya kuipeleka serikalini kwa kuwa hakuna mchango mwingine utakaopokelewa katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Bonyeza play hapa chini kutazama
ULIKOSA? ‘Umeme hakuna kupanda, majipu bado yapo na nitayatumbua’- Rais Magufuli, Bonyeza play hapa chini