Tunayo stori kuhusu Msitu wa Hifadhi Vikindu ambapo upo katika wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani ukiwa umeandaliwa kwa ajili ya shughuli za Kitalii kama ilivyo katika maeneo mengine.
Msitu huo una ukubwa wa hekari 1,681 na upo kilomita 17 kutoka katikati ya jiji la Dar es salaam ambapo inaelezwa kuwa vivutio vilivyopo katika msitu huo ni pamoja na mimea asilia na wanyama mbalimbali wakiwemo Mbega wenye rangi nyeupe na nyeusi (black and white colubus monkey), swala, ngiri, ngedere, kima na nyoka.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa hifadhi ya msitu huo, Meneja Msitu wa Wilaya Mkurunga, Christina Mohammed amesema kwa miaka michache iliyopita serikali iliyumba kuisimamia vizuri misitu ambapo ikisahaulika kidogo lazima ishambuliwe.
“Msitu wa Vikindu tulishakata tamaa na tuikasema tuuachie kwa matumizi mengine, kwani ukiangalia kwa hali halisi ya maendeleo ya mji wa Dar es Salaam unaona kuna hali ya hatari inayoweza kujitokeza kama hatutakuwa waangalifu,“amesema.