Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo July 13, 2017 ameahirisha kusikiliza kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Agnes Gerald ‘Masogange’ kwa sababu ya matatizo ya kiafya yanayomkabili mtuhumiwa huyo.
Wakili wa Serikali, Costantine Kakula alieleza shauri hilo la Masogange limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini hata hivyo, Wakili wa Masogane, Ruben Simwanza alimueleza Hakimu kwamba mteja wake anaumwa hivyo anaomba kesi iahirishwe ambapo Hakimu Mashauri aliahirisha hadi July 25, 2017 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.
Ulipofikia urejeshwaji wa mikopo ya elimu ya juu!!!