Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema mradi wa mafuta ghafi utasaidia kuongeza ajira kwa Watanzania na kuchochea utafutaji wa mafuta wa pamoja katika eneo la Afrika Mashariki.
“Kati ya kilomita 1,443 za bomba hili kilomita 1,147 zitapita Tanzania ndani ya Mikoa nane na Wilaya 24 naamini ajira nyingi zitazalishwa hapa, kama mnavyojua tuna deni la kuzalisha ajira zaidi ya milioni saba kwa miaka mitano hii, hivyo mradi huu utaongeza ajira,” Rais Samia
“Tanzania mbali na gawio la kuwa na hisa kwenye kampuni na kama ilivyosemwa hapa tumeingia kwa kiasi chote tulichomegewa asilimia 15, mbali na hiyo tutapata mapato ya kodi asilimia 60 mradi huu ni wa faida sana kwetu.” Rais Samia
“Utachochea shughuli za utafutaji pamoja mafuta na gesi kwa eneo letu la Afrika Mashariki tuna mategemeo ya kupata mafuta kupitia ziwa Eyasi na DRC na wenyewe wana mategemeo ya kupata mafuta na miundombinu itakayotumika ni hii ambayo tumekubaliana kujenga,” Rais Samia.