Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeazimia serikali inarejesha kiasi cha shilingi Bilioni 79.76 ya Mikopo iliyotolewa kwa vikundi vya Vijana,Wanawake na Wenye ulemavu
Azimio hilo limetolewa na mwenyekiti wa Kamati hiyo Halima Mdee wakati akisoma taarifa ya Kamati hiyo kuhusu ripoti ya CAG kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha ulioishia June 30,2023.
Mdee amesema “Mikopo inayotolewa katika vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu inapaswa kurejeshwa kwa wakati ulioainishwa katika mkataba wa makubaliano baina ya Halmashauri na vikundi ili vikundi vingine viweze kunufaika na mikopo hiyo.
Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Halmashauri zilitoa mikopo ya jumla ya Shilingi 73,411,018,877.
Hata hivyo, kutokana na ufuatiliji mdogo wa ukusanyaji wa mikopo hiyo, hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2023, Halmashauri zilishindwa kukusanya Shilingi Bilioni 79.76.” Halima Mdee